
Serikali imesema imesambaza vifaa zaidi ya Mil. 1.6, vya mtu kujipima mwenyewe maambukizi ya Virusi vya UKIMWI, kuanzia mwaka 2021.
.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Mhe.Ummy Mwalimu leo katika kilele cha Mdahalo wa Kitaifa wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania (NACOPHA), uliofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
.
Waziri Ummy amesema hatua hiyo imefikiwa kwa kushirikiana na Wizara ya TAMISEMI, huku akisisitiza kuongeza nguvu za kusambaza vifaa hivyo, ili kuweza kutambua hali zao wenyewe na kwa haraka zaidi.