Back to top

Serikali yasitisha makongamano na mikutano ya mkesha Disemba 31.

30 December 2020
Share

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.George Simbachawene amesema serikali imesitisha makongamano au mikutano ya mkesha katika maeneo yote ya wazi siku ya tarehe 31 Disemba mwaka huu katika mikoa yote kutokana na changamoto za kiusalama.

Mhe.Simbachawene ametoa tamko hilo la serikali jijini Dodoma ambapo amesema makongamano na mikutano hiyo ifanyike kwenye maeneo ya nyumba za ibada na mwisho iwe ni saa sita na nusu usiku.

Aidha katika hatua nyingine Mhe.Simbachawene amempongeza askari wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji wilayani Ngara mkoani Kagera kwa kitendo cha kishujaa cha kumuokoa mtoto aliyetupwa chooni.