
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, amemtupia lawama Makamu wa Rais wa Nchi hiyo, Rigathi Gachagua, kufuatia uvamizi uliotokea leo, Machi 27, 2023, katika shamba la familia ya Kenyatta lililopo kando ya Barabara ya Nairobi Eastern Bypass na kiwanda cha Odinga cha gesi cha East Africa Specter Limited, ambapo katika shamba la Kenyatta wavamizi hao wamekata miti na kuiba kondoo waliokuwepo kwenye shamba hilo.
.
Jambo la kushangaza ni kwamba hakuna Askari Polisi walioonekana kwenye eneo hilo tangu uvamizi huo, uanze mapema asubuhi, hatua iliyosababisha baadhi ya viongozi nchini humo kuihoji serikali kwa kushindwa kulinda mali za raia.
.
Kulingana na kiongozi huyo wa upinzani, Gachagua aliwafadhili majambazi hao kupigana na aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta, ambaye Naibu Rais alinukuliwa akisema ndiye aliyehusika na maandamano ya Azimio dhidi ya serikali.
