
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, ameongoza viongozi mbalimbali katika mapokezi ya ndege aina ya Airbus 320, yenye uwezo wa kubeba abiria 180 ya Shirika la Ndege la Saudia Arabia, ambayo kwa mara ya kwanza itaanza safari zake za moja kwa moja kutoka Dar es Salaam hadi Saudi Arabia, bila kutua katika nchi yoyote.
.
Ujio wa Shirika hilo utasaidia kuongeza pato la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), kukuza utalii na kupunguza muda wa safari kutoka saa takribani 10 mpaka saa 4 na nusu.
