Back to top

SPORT PESA KUOMBA FIDIA, JEZI MPYA YANGA

01 February 2023
Share

Kampuni ya mchezo wa kubahatisha ya SportPesa imetoa taarifa ya kusikitishwa na uamuzi uliochukuliwa na Uongozi wa klabu ya Soka ya Yanga, wa kukiuka makubaliano yao ya kimkataba na kuzindua jezi mpya zenye jina la mfadhili mwingine, ambapo kampuni hiyo imebainisha kuwa inahifadhi haki yake ya kuomba fidia na msaada kutoka kwa mamlaka husika kwa uharibifu uliosababishwa.