Back to top

Takriban watu milioni 1,422,951, duniani kote wafariki kwa Corona.

27 November 2020
Share

Virusi vya Corona vimesababisha vifo vya takriban watu milioni 1,422,951, duniani kote tangu kisa cha kwanza cha virusi hivyo kiliporipotiwa nchini China mwaka uliopita.

Mbali ya vifo hivyo watu milioni 60,427,590 wameambukizwa virusi hivyo vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19, kati ya hao watu wapatao milioni 38,532,900 wamepona.

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa, AFP.

Hata hivyo, idadi hiyo huenda ikawa kubwa zaidi tofauti na iliyotajwa kwani nchi nyingi hufanya vipimo kwa watu wenye dalili za ugonjwa huo.

Nchi iliyoathirika zaidi na janga la COVID-19 duniani ni Marekani, ikifuatiwa na Brazil nayo India ikishika nafasi ya tatu.