Back to top

TAKUKURU yawaomba wananchi kutoa taarifa za rushwa.

24 April 2018
Share

Kamanda wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa ( TAKUKURU), mkoa wa Lindi, Stephen Chami, amewaomba wananchi mkoani humo kuendelea kushirikiana na taasisi hiyo kwa kutoa taarifa pindi wanapokutana na vitendo vya rushwa kwenye maeneo yao.

Kamanda huyo wa Takukuru, amesema licha ya kujitaidi kuwaelimisha wananchi  lakini changamoto kubwa inayojitokeza kwa jamii bado kuna baadhi ya watu ni waoga kutoa taarifa Takukuru.