Back to top

TANZANIA INA WAGONJWA 54 WA SURUA NA LUBELA

15 September 2022
Share

Wizara ya Afya imethibitisha kuibuka kwa ugonjwa wa Surua na Lubela hapa nchini na kubainisha mpaka sasa wagonjwa 54 kutoka mikoa mbalimbali wamethibitika kuwa na ugonjwa huo.

Waziri wa Afya, Mhe.Ummy Mwalimu akiwa jijini Dodoma amesema Halmashauri 7 zikiwa na wagonjwa wengi na kati ya wagonjwa hao, 48 ni watoto chini ya miaka 15 na wagonjwa 6 ni walio na umri wa zaidi ya miaka 15.

Mhe.Ummy amesema hakuna taarifa ya kifo iliyoripotiwa na kuwataka wananchi kuendelea kuchukua hadhari.

Waziri Ummy pia amesema serikali imefuatilia suala la kuibuka kwa ugonjwa huo na kubaini kuwa watoto  Laki- Nne waliochini ya miaka mitano hawajapata chanjo ya ugonjwa huo na wengine kushindwa kukamilisha chanjo.