Back to top

Tanzania kutumia simu za mkononi kuinua sekta ya bima nchini.

21 August 2018
Share

Mamlaka ya uthibti wa bima kwa kushirikiana na serikali imejipanga kutumia fursa ya mawasiliano ya watumiaji wa simu za mkononi katika kuongeza wigo wa wateja katika soko la bima ili kuongeza mchango wa sekta ya bima katika pato la taifa na kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi chache duniani zinazotegemea bima katika pato la taifa.

Akizungumza kuhusu mkutano 41 wa kimataifa wa sekta ya bima utakayojumisha zaidi ya mataifa 30 unaofanyika nchini, kamishna wa bima Daktari Baghayo Saqware licha ya sekta ya bima hapa nchini kuwa imara bado mchango wa sekta ya bima katika pato la taifa ni asilimia moja, tofauti na Kenya asilimia 3.5 aambapo kupitia mkutano huo sekta ya bima nchini inatarajia kukuza soko pamoja na uwezo wa kitaaluma na kimtaji miongoni mwa makampuni ya bima hapa nchni.

Mwenyekiti wa kamati ya mkutano wa Kimataifa Bwana. Hamisi Selemani amesema takwimu zinaonesha mpaka sasa ni asilimia 15 ya watanzania ndio wako kwenye mifumo ya bima kupitia mkuatno huo wanalenga kutumia uzoefu nchini zitakazoshiriki katika kukuza uwezo wa sekta ya bima nchni ili kuongeza ajira na pato la taifa kwa kuwafikia watu wengi zaidi.