Back to top

TANZANIA YAPATA MKOPO NAFUU BENKI YA DUNIA

28 February 2023
Share

Serikali ya Tanzania na Benki kuu ya Dunia, zimesaini mkopo nafuu utakaosaidia kuboresha utoaji na upatikanaji wa huduma za afya nchini , ikiwemo kupunguza vifo vya mama na mtoto,kuboresha huduma za dharura na ufanisi wa huduma katika ngazi ya zahanati.
.
Hafla hiyo imeongozwa na Waziri wa fedha na mipango nchini Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Afya bara Dkt. Godwin Mollel aliyemwakilisha Waziri wa Afya pamoja na mwakilishi kutoka Serikali ya Zanzibar Mhe. Amur Mohamed.