Taasisi ya Utafiti wa Kilimo nchini (TARI) kituo cha Uyole inakusudia kutoa bure mbegu za mazao ya aina mbalimbali kwa wakulima watakaotembelea banda la taasisi hiyo kwenye viwanja vya maonyesho ya kilimo Nanenane jijini Mbeya.
Afisa Ughani wa TARI kituo cha Uyole, Nyimila Barton Kalindile ameyasema hayo wakati wa maandalizi ya mwisho ya banda la maonyesho la taasisi hiyo kwenye viwanja vya Nanenane vya John Mwakangale.
Mkurugenzi wa Taasisi hiyo kituo cha Uyole, Dk. Tulole Lugendo Bucheyeki amesema taasisi yake imeongeza idadi za mbegu mpya za mazao ya aina mbalimbali ambazo zitaonyeshwa kwa wananchi kwa mara ya kwanza wakati wa maonyesho ya kilimo ya mwaka huu ambayo yataanza kesho.