Back to top

TBS: DAWA ZA MENO HAZINA VICHOCHEO VYENYE ATHARI

02 April 2023
Share

Shirika la Viwango nchini (TBS) limesema dawa za meno zinazotolewa kama msaada kwenye baadhi ya shule hapa nchini hazina vichocheo vya kibiolojia (hormones) vinavyoathiri watuamiaji hasa watoto wa kiume.
.
TBS imetoa taarifa hiyo kufuatia taarifa zilizokuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa shirika hilo lilipima na kuthibitisha kuwa dawa hizo zina viambata hivyo ambapo limebainisha kuwa limefanya uchunguzi wa awali na kugundua kuwa hakuna uwepo wa vichocheo hivyo.
.
Hata hivyo shirika hilo linaendelea na kufuatilia suala hilo kwa kushirikiana na maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali