
Rais wa zamani wa Marekani Bw.Donald Trump, mwenye miaka 76, ameshtakiwa kwa kuhifadhi nyaraka za siri zilizoainishwa bila kibali
baada ya kuondoka Ikulu kama Rais wa nchi hiyo.
Wakili wa Bw.Trump Jim Trusty, ameambia shirika la habari la CNN kuwa rais huyo wa zamani alikuwa amepokea maelezo ya mashtaka katika hati ya wito.
Hata hivyo inaelezwa kuwa maofisa wa ujasusi wa siri watakutana na wasimamizi wa sheria ili kupanga safari ya Bw Trump hadi mahakama ya Miami katika siku zijazo.
Aidha Trump amekuwa akifanya kampeni ya kurudi Ikulu mnamo 2024.
