Back to top

"Tukahakikishe tunafanya kazi kwa matokeo yanayoonekana”.Dkt. Kijaji

14 September 2021
Share

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa watendaji wa wizara hiyo wanatakiwa kutekeleza wajibu wao kwa ufanisi mkubwa kwa kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi kwa sababu umma wa Watanzania una uchu wa kusikia kinachoendelea duniani hivyo kabla ya kufungia chombo chochote cha habari ni vema kutekeleza wajibu kwanza.

“Mifumo yote ya Taifa hili ipo chini ya wizara hii na tumeunganishwa na Sekta ya Habari, twendeni tukahakikishe tunafanya kazi kwa matokeo yanayoonekana”.Dkt. Ashatu Kijaji

Hayo ameyazungumza Dkt. Kijaji katika kikao chake cha kwanza na Menejimenti ya Wizara hiyo kilichofanyika katika ofisi za Wizara zilizopo Mtumba Dodoma.

Amesema kuwa matarajio yake ni kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na upendo baina ya viongozi wa wizara hiyo bila kusuguana kwa kufuata utaratibu wa utumishi wa umma ikiwemo kutunza siri za Serikali na kutoa taarifa sahihi kwa umma.