Back to top

TULIKWENDA KUFUFUKIA UGANDA - AHMED ALLY

03 March 2023
Share

Msemaji wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema timu hiyo imefufukia Uganda baada ya kuipiga Viper goli moja bila, ambapo amebainisha kuwa katika mechi inayofuata ambayo ni marudiano na timu ya Viper wanakwenda kuamua hatma ya timu hiyo kwenye michuano ya CAF. 
.
"Hatupo tayari kuishia hatua ya makundi. Tulikwenda kuchukua alama tatu kwa Vipers lakini hatujamaliza, tunakwenda kuzichukua alama zingine hapa nyumbani. Niseme tu tuko tayari kwa mchezo" Ahmed Ally.

Ahmed ameyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari huku akisisitiza kuwa hawako tayari kuishia hatua ya makundi.
.
"Tulikwenda kufufukia Uganda, na kweli tumefufuka. Jumanne ni mechi ya marudio katika mechi hii tunakwenda kuamua hatma ya Simba kwenye michuano ya CAF. Tukimpiga tutafikisha alama 6 na kuanza kuchungulia robo fainali" Ahmed Ally.