
Tume ya madini Tanzania kwa mujibu wa sheria ya madini ya mwaka 2010 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2017 na kanuni za madini imezifuta jumla ya leseni 11 za uchimbaji wa madini katika migodi mikubwa na midogo nchini kutokana na wamiliki wa leseni hizo kuhodhi maeneo bila ya kuyaendeleza ambapo leseni hizo zimerudishwa serikalini bila hakikisho la kupewa tena.
Akizungumza mkoani Dodoma Mwenyekiti wa Tume ya madini nchini Prof.Idris kikula amesema kurudishwa leseni hizo serikalini ni matakwa ya kisheria ambapo amesema kila Mtanzania anapaswa kunufaika na rasilimali za madini ili kuinua uchumi wa nchi.
Kwa upande wake Kamishna wa Tume hiyo Atanas Macheyeki amesema hakuna ubaguzi katika utoaji wa leseni kwa wachimbaji wadogo na kwamba sheria inawatambua na kuna vigezo vinavyozingatiwa katika uombaji wa lkeseni na ni haki ya kila mwananchi kupata leseni.
Naye Katibu Mtendaji wa Tume ya madini Prof Shukrani Manya amesema sababu iliyopelekea kufutwa kwa leseni hizo ni kutokana na baadhi ya makampuni kuhodhi bila ya kuyaendeleza ambapo sheria imeziondoa leseni hizo za kuhodhi na kuzirudisha serikalini.