Back to top

Uchakavu wa mitambo ya kufua umeme Hale, Korogwe wamtisha Dr.Kalemani.

18 October 2019
Share


Mitambo ya kufua umeme katika kituo cha kufua Nishati hiyo kilichoko Hale wilayani Korogwe imeharibika kutokana na uchakavu na kusababisha kushindwa kushindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Akizungumza baada ya Waziri wa Nishati Dr.Medard Kalemani kufika katika kituo hicho kukagua mitambo hiyo, Kaimu Meneja Mhandisi Jackline Mtolela amesema hivi sasa kituo kinafua megawati nane  badala ya ishirini na moja zinazotakiwa.

Kufuatia hali hiyo Waziri wa Nishati Dr.Kalemani amewapa siku tatu watendaji wa kituo hicho wahakikishe mashine moja kati ya mbili zinazotumika inatengemaa na kuanza kufua megawati kumi nukta tano na kuutaka uongozi kumtafuta mkandarasi haraka kwa ajili ya kutengeneza mashine zote ili ufuaji wa umeme ufikie megawats 21.

Dr.Kalemani pia amezindua mradi wa umeme katika vijiji vya Mwandusi na Mtundani vilivyoko wilayani Mkinga ambako amewataka wananchi wawafichue wanaohujumu miundombinu ya umeme.