Back to top

Uchimbaji mchanga wahatarisha usalama wa mazingira.

17 October 2018
Share

Licha ya kuwepo agizo la kuzuia uchimbaji holela wa michanga ndani ya mto ya jiji la Dare es salaam ikiwemo mto Mpiji unaotenganisha Mkoa wa Dar es Salaam na mkoa wa Pwani kwa upande wa wilaya ya Kinondoni vitendo hivyo vimeelezwa kuendelea na kuhatarisha usalama na mazingira.

Wakizungumza na ITV baadhi wananchi wanaoishi kando kando ya mto Mpiji wameeleza pamoja na kuwepo tishio ya mvua kubwa wamekuwa wakijitokeza watu wakidai kuwa na vibali vya kusafisha mito kutoka ofisi za bonde la Ruvu huku wakizindi kuupanua na kuharibu kingo zake kuelekea kwenye makazi ya watu siku hadi siku.

ITV imeshuhudia baadhi ya makampuni yanayochimba michanga katika mto huo wa Mpiji kwa kutumia mashine za kisasa ambao kwa masharti ya kutopigwa picha wala kutajwa majina yao wanaeleza kuwa na vibali vyote husika katika kufanya kazi hiyo.

Aidha ITV imewatafuta maofisa wa bonde kwa njia ya simu na kumpata afisa aliyejitambulisha kwa jina moja la mshuda ambaye pamoja na kueleza kutokuwa msemaji wa ofisi ya bonde anakiri ofisi kutoa vibali kwa kampuni tatu katika mto huo ambazo zimepewa utaratibu wa kusafisha kwa kuepuka kupanua mto akiahidi kufuatilia endapo wamekiuka utaratibu huo.