
Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Habib Nsikonnene (43) kutoka kijiji cha Namasengere katika Wilaya ya Mukono nchini Uganda amegonga vichwa vya habari nchini humo baada ya kufunga ndoa na wanawake saba kwa siku moja, na miongoni mwa wake zake wawili ni ndugu wa damu.
Inasemekana kuwa msafara wake wa ndoa ulikuwa na takriban magari 40 na pikipiki 30 ambapo kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa biashara ya Nsikonnene inaingiza pesa nyingi.
Nsikonnene, ambaye anasemekana kuwa na uwezo kipesa katika eneo hilo na anatarajiwa kuandaa sherehe kubwa ya mapokezi ya wake zake wote saba siku ya Jumapili na kualika