
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy, ameituhumu Urusi kwa kufanya uhalifu wa kivita na kuwauWa raia huko Kherson, katika baadhi ya maeneo ambayo yalirudi katika udhibiti wa Ukraine wiki iliyopita baada ya Urusi kuondoka.
Wachunguzi tayari wamesharekodi zaidi ya visa 400, vya uhalifu wa kivita uliofanywa na Urusi, miili ya raia na majeshi imepatikana ingawa Urusi imekanusha kwamba vikosi vyake vilikusudia kuwalenga raia katika mashambulizi yake.
Katika eneo la Kherson, Jeshi la Urusi lilifanya unyama kama lilivyofanya katika sehemu zengine za nchi yetu ilizofanikiwa kuzivamia.
Makaburi ya halaiki yamegunduliwa katika maeneo kadhaa kote nchini Ukraine, tangu mwanzo wa uvamizi huo Februari 24, ikiwemo miili ya raia iliyokuwa na ushahidi wa kuteswa katika maeneo la Kharkiv na Bucha karibu na Kyiv.
