Back to top

UNDP:Tanzania uenda ikashindwa kufikia SDGs.

20 March 2019
Share

Shirika la maendeleo la umoja wa mataifa (UNDP) limesema Tanzania uenda ikashindwa kufikia malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kumi na saba kama haitatatua changamoto ya ukosefu wa ajira, uharibifu wa mazingira pamoja na usawa wa kijinsia unaochangiwa kwa kiasi kikubwa na miradi na tamaduni potofu.

Akizungumza na vyombo vya habari, katika mkutano unaojumuisha mabalozi,wadau wa maendeleo na sekta binafsi wenye lengo la kuchochea sekta binafsi kushiriki katika mpango wa maendeleo endelevu, Bwana mwakilishi mkazi wa Shirika la maendeleo la umoja wa matifa (UNDP) Bwana Alvaro Rodriuez amesema moja ya changamoto kubwa inayoikabili Tanzania ni usawa wa kijinsia kati ya wanawake, wasichana dhidi ya wanaume na wavulana.

Mwenyekiti wa jukwaa la wadau wa maendeleo linaloratibiwa na umoja wa mataifa, Bwana Saimon Shayo amesema ili kufikiwa kwa malengo hayo serikali inapaswa kutoa fursa kwa sekta binafsi kuchangia kutegeneza ajira endelevu zitakazosaidia kuwashirikisha watanzania kuchangia katika uchumi wa nchi yao pamoja na kuwaondoa katika umasikini.

Akielezea serikali inayotekeleza malengo ya maendeleo endelevu, Mkurugenzi wa wizara ya fedha na mipango Bwana Servu Sagdai amesema serikali imeweka miundombinu ya utekelezaji wa malengo ya (SDGs) .ambapo baadhi ya malengo hayo yanatekelezwa kupitia mpango wa maendeleo ya miaka mitano, huku mkurugenzi wa taasisi ya sekta binafsi godfrey simbeye akisisitiza asilimia 70 ya ajira rasmi zinatolewa na sekta binafsi.