Back to top

USAFIRISHAJI WAHAMIAJI HARAMU, POLISI 5 MBARONI

03 November 2022
Share

Askari watano wa Jeshi la Polisi Mbeya, wamekamatwa wakisafirisha wahamiaji haramu kwenda nchini Malawi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Benjamin Kuzaga, amesema askari hao walikamatwa eneo la Uyole Jijini Mbeya, wakiwa na wahamiaji hao haramu wakijiandaa kuwasafirisha.

Ameongeza kuwa, askari hao walikuwa na gari dogo aina ya Toyota Cresta, lenye namba za usajili T.946 BTT mali ya askari mmojawapo, ambalo walikuwa wamewabeba wahamiaji hao, tayari kwa safari ya kuelekea wilayani Kyela, mpakani mwa Tanzania na Malawi.