Back to top

Vyeti vya kuzaliwa sasa kutolewa bure kuanzia ngazi ya kata.

18 September 2018
Share

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umeanza kutekeleza Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa bure kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano huku mkoa wa Kigoma ukiwa na kiwango cha asilimia 8.1 pekee cha watoto waliosajiliwa kiwango kinachotajwa kuwa kidogo zaidi ukilinganisha na mikoa mingine ya Tanzania Bara.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bi.Emmy Hudson amesema mpango huo ambao umekwishaanza kutekelezwa katika baadhi ya mikoa hapa nchini utasaidia kuondoa changamoto na usumbufu unaosababisha wazazi kushindwa kupata vyeti vya watoto na kwamba usajili utafanyika bure katika vituo vya kutolea huduma za afya na ofisi za kata.