Back to top

WABUNGE SUKUMENI BIMA YA AFYA KWA WOTE

19 April 2023
Share

Serikali imewataka wabunge kutosubili mswada wa Bima ya Afya kwa Wote, bali wawe sehemu ya kuusukuma mswada huo upite ili kila mwananchi aweze kunufaika na huduma za afya katika ngazi zote kuanzia zahanati mpaka hospitali ya taifa bila malipo. 
.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt.Godwin Mollel, leo Aprili 19, 2023 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Mhe. Asia Halamga, ambapo amebainisha kuwa endapo mpango huo utakamilika, utakuwa suluhisho la upatikanaji wa huduma za afya kwa makundi yote ya kijamii wakiwemo wafungwa.