Back to top

Wachimbaji madini waiomba serikali kuangalia upya sheria ya madini

05 February 2019
Share

Wachimbaji wa madini mkoani Katavi wameiomba serikali kuangalia upya sheria ya madini na ikiwezekana itengenezwe sheria mpya itakayoangalia upatikanaji wa madini kwa kanda, kutokana na mkoa wa Katavi kuzalisha madini aina ya shaba,fedha na dhahabu katika mwamba mmoja hali inayopelekea kazi ya uchenjuaji wa makinikia kuwa ngumu na hivyo kusababisha madini mengi kupotea
 
Wachimbaji hao wametoa ombi hilo katika mkutano uliokutanisha wadau mbalimbali wa madini
 
Akizungumza na wachimbaji hao afisa madini mkazi mkoa wa Katavi Sudian Chiragwile amewataka wadau hao kuangalia fursa kwa rasilimali zilizopo hasa za madini ya ujenzi na kuingiza teknolojia za kisasa ili kuwezesha utengenezaji wa vifaa mbalimbali
 
Naye mkuu wa mkoa wa Katavi Amos Makala amewataka wachimbaji na wauzaji wa madini kuunga mkono jitihada za serikali katika kuinua mapato yatokanayo na madini