Back to top

Wachimbaji Mererani wadaiwa kuanza kuruka ukuta.

15 January 2019
Share

Afisa Madini mkazi Mererani Daud Ntalima amesema wameanza msako kuwadhibiti baadhi ya wachimbaji wadogo wanaofanyakazi mgodi wa mererani ambao wanaruka ukuta na kufanya uhalifu ndani ya mgodi.

Baadhi ya wachimbaji  na viongozi wa serikali za vijiji vinavyozunguka migodi hiyo wanaunga mkono kuchukuliwa hatua kwa watu hao huku wakiitaka serikali kupunguza  vikwazo vilivyopo kwenye migodi hiyo kwa kuwa viimekuwa chanzo cha baadhi ya wachimbaji kukiuka taratibu.