Back to top

Wachimbaji wadogo waiomba serikali iwashirikishe ugawaji wa Vitalu.

03 April 2018
Share

Wachimbaji wadogo kutoka mikoa mbalimbali nchini wameiomba serikali kuwashirikisha kabla ya kugawa Vitalu kwa wawekezaji pamoja na kutunga sheria na kanuni za uchimbaji kwa sababu sehemu kubwa ya wachimbaji hawana elimu ili waweze kulipa kodi badala ya kutumia nguvu katika zoezi la kuwaondosha.

Wakizungumza mjini Morogoro mara baada ya wadau wa sekta ya madini kukutana na wachimbaji hao kujua changamoto na jinsi ya kukabiliana nazo,wachimbaji hao wamesema ni vyema kabla ya serikali haijakaa na kutunga sera na sheria za madini ingewashirikisha kwa sababu wao ndio wagunduzi wa madini nchini.

Kuhusu thamani ya madini kushuka,mtaalam wa madini nchini Boco Tindebwa amesema madini yanayouzwa nje ya nchi yananunuliwa kwa fedha kidogo kwa sababu yanachimbwa bila kuzingatia utaalam sanjari na kukosa kiwanda cha kuchonga madini.

Kufuatia hatua hiyo Mjiolojia kutoka shirika la madini la taifa (STAMICO) Denies Silas amesema tayari serikali imeanza mchakato wa kuwashirikisha wachimbaji katika mambo tofauti ikiemo elimu na dhamana ya kupata mikopo.