Back to top

Wafugaji wa nyuki Mbozi waomba msaada wakitaalamu kudhibiti siafu.

05 June 2018
Share

Wafugaji wa nyuki katika msitu wa Ilembo wilayani Mbozi mkoa wa Songwe wameiomba serikali kuwapa ushauri wa kitaalam utakaowawezesha kukabiliana na siafu waharibifu  wanaoshambulia mizinga,kuua nyuki na kula asali hali inayopelekea uzalishaji wa asali kudorola kutoka tani moja hadi lita 800 kwa mwaka.

Wakizungumza na ITV wafugaji hao walijiundia kikundi cha ujasiriamali cha UWUSHI,wameunganisha changamoto ya sisimizi kuvamia mizinga na nyingine ya watu wasiojulikana kuvamia na kuimba mizinga ya kisasa na asali jambo linalosababisha malengo ya wafugaji hao kutotimia.

Kufuatia changamoto hiyo Mkuu wa wilaya ya Mbozi John Palingo ameongozana na  wataalamu wa nyuki  kutoka Ofisi za wakala wa misitu wa wilaya hiyo na kufika kwenye msitu wa Ilembo ambapo Afisa nyuki Bi.Dorice Kilahama amesema hakuna njia ya kisasa ya kukabiliana ya wadudu hao isipokuwa kwa kutumia Oil chafu na kuning'iniza  mizinga kwa kutumia waya badala ya kamba, njia iliyozoeleka na wengi.

Lengo la kikundi cha UWUSHI ni mizinga 40 kuzalisha zaidi ya tani moja kwa mwaka,lakini changamoto hizo mbili zimepelekea kushuka kwa uvunaji hadi lita 800 kwa mwaka.