Back to top

WAJAZA MCHANGA KWENYE MIFUKO 776 YA MBOLEA

05 March 2023
Share

Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, ameagiza kukamatwa na kuhojiwa kwa Viongozi wa Kampuni ya Minjingu akiwemo Meneja Masoko wa kampuni hiyo Dkt.Mshindo Msola, pamoja na Viongozi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Nchini (TFRA) baada ya mifuko 776 ya mbolea ya kampuni hiyo kukutwa ikiwa imejazwa mchanga katika ghala la kampuni hiyo lililopo mjini Njombe, tayari kwa kuuzwa kwa wakulima.