Back to top

WAKAGUZI ELIMU, KAGUENI KINACHOENDELEA SHULE ZA BWENI

14 February 2023
Share

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza Wakaguzi wa Elimu, kwenda kufanya ukaguzi katika shule ili kujionea ambacho wanafunzi wanafundishwa na kujifunza ikiwa ni pamoja na kukagua vitabu vinavyotumika na kinachoendelea kwenye mabweni yanayotumiwa na wanafunzi hao, kutokana na kuwepo kwa baadhi ya vitabu vyenye mafundisho yasiyoendana na mila na desturi za kitanzania.    
.
Mhe.Majaliwa ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Songwe, akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa mkoani Songwe.