Back to top

WAKULIMA 5,385 WANUFAIKA NA MKOPO WA BIL.164.9

31 January 2023
Share

Waziri wa Fedha, Mhe.Mwigulu Nchemba amesema kuwa hadi kufikia Disemba 31, 2022, wakulima wadogo 5,385 pamoja na AMCOS 21, wamenufaika na mkopo wa Tsh. Bil.164.9 uliotolewa na Serikali kupitia Benki Kuu (BoT) kwa benki na taasisi za fedha nchini ili kuboresha mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo cha mazao, miundombinu ya umwagiliaji, mifugo, uvuvi na ununuzi na usindikaji wa mazao yake kwa wakulima wadogo na wa kati na kampuni ndogo ndogo na za kati.
.
Mhe.Mwigulu ameyasema hayo Bungeni leo Januari 31, 2023, Bungeni Jijini  Dodoma.