
Wakulima wa zao la Pamba, mkoani Geita wamedai wanalazimika, kufuata mbolea ya ruzuku na pembejeo, mkoani Shinyanga kutokana na kukosekana kwa mbolea kwenye maeneo yao, hali inayosababisha wakulima kuingia gharama kubwa katika usafirishaji ambapo wameiomba serikali kuwapelekea mbolea kwenye maeneo yao ili kuondoa usumbufu huo.
.
Wakulima hao wameyasema hayo wakati wakijadili changamoto zinazowakabili kwenye maeneo yao ambapo pia wamedai upatikanaji wa mbegu nao umekuwa tatizo.
