Back to top

Wakulima wa Mpunga wilayani Tunduru waomba serikali kudhibiti ununuzi.

22 April 2019
Share

Baadhi ya wakulima wa zao la Mpunga katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, wameiomba serikali wilayani humo kuwa na mfumo thabiti wa kusimamia na kudhibiti ununuzi holela wa zao la Mpunga ili wakulima wengi waweze kunufaika na bei nzuri ya zao hilo.
     
Wakulima hao wametoa ombi hilo katika kikao cha pamoja kati yao na mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Bw. Juma Homera wakati akitangaza msimamo wa serikali kuhusu ukusanyaji na ununuzi wa zao hilo kupitia mfumo wa maghala tofauti na ilivyo sasa ambapo wakulima wanauza Mpunga wao holela kwa bei zisizo na tija.

Akitoa msimamo wa serikali kuhusu mfumo huo, mkuu huyo wa wilaya ya Tunduru, Bw. Juma Homera amesema wamejipanga kudhibiti ununuzi holela wa zao la Mpunga kwa wakulima na kwamba watahakikisha wanaendesha msako  na kuwakamata wafanyabiashara wote watakaokiuka mfumo huo.