Idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa homa ya Corona nchini Uganda yafikia 18.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii ameandika kwamba watu wengine 4 wameambukizwa na kirusi cha Corona na kufanya idadi ya wagonjwa kufikia 18.
Museveni amesema watu hao 4 ni miongoni mwa raia waliosafiri kutoka Dubai na kuwekwa karatini.