Back to top

WALIOPEWA MIKOPO SAME WASUASUA KUREJESHA

12 March 2023
Share

Mkuu wa Wilaya ya Same, Bi.Kasilda Mgeni amesema zaidi ya shilingi bil.1 zilizokopeshwa kwenye vikundi vya wanawake, ikiwa ni mikopo ya 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo, yenye lengo la kuviwezesha vikundi hivyo kujikwamua kiuchumi, vimetajwa kusuasua kurejesha mikopo hiyo hali ambayo inadaiwa kukwamisha juhudi za Halmashauri hiyo, kuvifikia vikundi vingine vyenye uhitaji.
.
Bi.Mgeni ameyasema hayo wakati akizungumza na wanawake wilayani humo ambapo amesema, endapo havitarejesha mikopo hiyo serikali haitasita kuvichukulia hatua.