Back to top

Wamiliki wa Bodaboda watakiwa kukatia bima vyombo hivyo vya Usafiri.

02 November 2022
Share

Wamiliki wa pikipiki maarufu kama (Bodaboda) mkoani Morogoro wametakiwa kuwakabidhi pikipiki madereva wenye leseni pamoja na kukatia bima vyombo hivyo ili kuwasaidia wahanga wa ajali zinazotokana na pikipiki kuweza kupata fidia.

Hayo yambanishwa na Kamanda wa Usalama Barabarani mkoani Morogoro SSP Zauda Mohamed mara baada ya utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya usalama barabarani, ambapo amesema kumekuwepo na matukio ajali za bodaboda zinazotokana na madereva wa vyombo hivyo kutokuwa na leseni.

Katika hatua nyingine SSP Zauda  Mohamed amesema ni vizuri wamiliki wa pikipiki kuhakikisha wanakuwa na bima za vyombo hivyo ili kuwasaidia madereva wa bodaboda pindi wanapopata ajali kupata fidia.

Nao baadhi ya wanufaika wa elimu wamesema kutokana na elimu hiyo wamejifunza namna ya kuchukua tahadhari wakati wanatumia vyombo hivyo kwenye usafiri

Kutokana na hali hiyo madereva wa pikipiki wamesema bima zina umuhimu mkubwa kutokana na kumsaidia dereva kupata haki zake pindi anapopata ajali