
Wananchi wa Kijiji cha Chitanda, Kata ya Newala mkoani Mtwara, wamepata maji safi na salama jambo ambalo wamesema hatua hiyo sasa inawaepusha na kukimbizwa na wanyama wakali wanapoenda kufuata maji katika maeneo yenye bonde.
Mbali nawao kufuata maji wamesema pia imesaidia kusaidia watoto kuweza kuhudhuria masomo vizuri, pamoja na kuwaepusha na vitendo vya ukatili.
Mhandisi wa maji kutoka Newala, Juma Hassani amesema mradi huo wa Chitandi mbali na kuhudumia wakazi wa Kijiji cha Chitandi zaidi ya 1800, lakini pia baadhi ya wakazi wa mji wa Newala watafaidika na mradi huo.
Mhandisi Juma ameeleza kuwa miradi inayotekeleezwa mpaka hivi sasa kwenye Wilaya hiyo, ni kumi na mbili yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 6, ambapo lengo la serikali ni kuona wananchi wote wa wilayani Newala wanapata maji safi na salama.
