Back to top

WANANCHI WAPEWA ELIMU YA MFUKO HIFADHI YA JAMII

07 August 2024
Share

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Abdul-Razaq Badru, amewaongoza watumishi wa mfuko huo kutoa huduma na elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Wanachama na Wananchi wanaotembelea banda la Mfuko kwenye viwanja vya Nzuguni Dodoma ambako maonesho hayo yanafanyika kitaifa.

Huduma kama hizo zimekuwa zikitolewa na Maafisa wa PSSSF kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea kwenye Kanda za Nyanda za Juu Kusini katika viwanja vya John Mwakangale, Jijini Mbeya na kwenye viwanja vya Dole Kisiwani Unguja, Zanzibar.
“Siku zote tumekuwa tunasema Leo, Kesho Pamoja, hivyo tuko hapa, kuwahudumia wanachama wetu, tupo katika mkakati maalum wa kufanya shughuli zetu kidigitali, Wastaafu wanajihakiki kidijitali, wanachama wanatazama taarifa zao kidijitali.” Amesema Badru.

Amesema Mfuko pia umejitanua zaidi kwa kunanadisha shughuli inazofanya ambazo zinaunganisha Mfuko na Jamii za Wafugaji na Wakulima kupitia uwekezaji kwenye vitegauchumi vya viwanda vya Ngozi na viatu Kilimanjaro, Machinjio ya Nguru Hills Ranch Mvomero, ambavyo vimetoa fursa kwa wafugaji.
Pia kiwanda cha kuchakata Tangawizi kilichoko Mamba Miamba Wilayani Same, Mkoani Kilimanjaro, Viwanda hivi ni fursa kwa wakulima, amesema Bw. Badru.