
Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Wilaya ya Songwe, imesema imeanza kuwachukulia hatua za kisheria na kuwaonya, baadhi ya wanunuzi wanakaoidi kudai risiti pindi wanaponunua bidhaa huku ikisisitiza kuendelea kutoa elimu kwa kundi hilo juu ya umuhimu wa kudai risiti.
.
Akizungumza na ITV, Kaimu Meneja wa TRA, Wilaya ya Songwe, Bw.Elinaza Daniel, amebainisha kuwa sheria inamtaka mnunuaji kudai risiti pindi anaponunua bidhaa, kinyume na hivyo ni kuvunja sheria.
.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Bw. Solomon Itunda, aliyeongoza zoezi la utoaji elimu hiyo, amewataka amewataka wananchi kuunga mkono jitihada hizo, huku akiwaomba TRA kuhakikisha wanafikisha elimu hiyo maeneo ya pembezoni.