Back to top

"WANAWAKE HUKATILIWA WAKATI WA UCHAGUZI"

01 December 2023
Share

Mkurugenzi WiLDAF Tanzania Anna Kulaya, amesema wanawake wengi hukatiliwa kwenye siasa wakati wa uchaguzi kwenye majukwaa na hata michakato ya ndani ya vyama vya siasa ya kuwafanya wawepo kwenye nafasi ya uongozi, mfano viti maalumu au kwenye majukwaa ya kisiasa wakati wa Kampeni.

Ameeleza hayo Jijini Dar es Salaam,  wakati wa mkutano wa uchambuzi wa miswada ya sheria za Uchaguzi, vyama vya siasa na Tume huru ya uchaguzi uliofanywa na umoja wa wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa ambapo walipendekeza kuwapo kwa vifungu vutakavyozuia ukatili kwa wanawake kwa namna yoyote ile.

Kwenye taarifa ya uchambuzi huo umebainisha kuwa vyama vingi vya siasa kwa sasa vina mfumo dume na hata viongozi wengi wa ngazi za maamuzi ni wanaume na hivyo wanawake kuendelea kuminywa katika haki zao za kisiasa.