Back to top

WANAWAKE NEC WATOA MSAADA KWA WAFUNGWA

03 March 2023
Share

Wafanyakazi wanawake wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wametoa msaada kwa wafungwa na mahabusu wanawake, waliopo Gereza kuu la Isanga Jijini Dodoma.
.
Akizungumza baada ya kutoa msaada huo, Mwenyekiti wa wanawake TUGHE, tawi la Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi.Nuwia Sultan ,amesema msaada huo  ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani Machi 8, 2023.