Back to top

Wanne wakamatwa Kagera baada ya kukutwa na magunia 31 ya bangi.

07 April 2019
Share

Watu wanne mkoani Kagera ambao ni wakazi wa  kilichoko katika kijiji Rwakilinda kilichoko wilayani Biharamulo  wanashikiliwa na Jeshi la polisi katika mkoa huo kwa tuhuma ya kukutwa na magunia 31 ya madawa ya kulevya aina ya bangi waliokuwa wameificha kwenye nyumba zao.

Akizungumza wakati akionyesha magunia ya bangi iliyokamatwa,Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Kamishina msaidizi, Revocatus Malimi amewataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Samwel Alexander, Andrea Wamala, Sabera Ndimjea na Leah Fabian, amesema bangi hiyo imekamatwa kufuatia operesheni mbalimbali zinazoendesha katika mkoa huo za kupambana na uhalifu na watuhumiwa hao walikuwa na mpango wa kuisafirisha hadi mkoani Mwanza.