Back to top

WASHTAKIWA KWA KUPUNGUZA UMRI NCHINI UGANDA.

28 March 2023
Share

Benki ya Uganda, imewashtaki wafanyakazi wa zamani na wa sasa juu ya hatua ya wafanyakazi hao, kupunguza umri wao ili kurefusha mikataba  yao na kuendelea kupokea pensheni na marupurupu mengine kutoka Benki Kuu.

Nyaraka zilizoonekana zinaonyesha baadhi ya wafanyakazi wa BoU, walipunguza umri wao kwa zaidi ya miaka minne. Wakati akifungua kesi hiyo, wafanyakazi 69 kati ya 77 walioshtakiwa walikuwa bado ni wafanyakazi hai wa benki hiyo huku wengine wakiwa ni waajiriwa wa zamani.

Benki ya Uganda inadai kuwa wafanyakazi hao 77 walitumia fursa ya kutangazwa kwa Sheria ya Usajili wa Watu, Namba 4 ya 2015 kupunguza umri wao wakati wa kujiandikisha kwa ajili ya vitambulisho vya taifa kinyume na kumbukumbu walizowasilisha benki mwanzoni mwa ajira zao.