Back to top

WASIO NA BIMA WALA FEDHA WAPATIWE HUDUMA KWANZA

01 February 2023
Share

Naibu Waziri wa Afya Mhe.Godwin Molel, amewataka watoa huduma za afya, kutathmini maisha ya watu kwa kutoa huduma kwanza hata kama muhusika hana bima ya Afya wala fedha za kulipia.

Aidha ameagiza hospitali zote za umma kuwa na dawa za kutibu ugonjwa wa kichaa cha mbwa. 

Mhe.Molel ametoa kauli hiyo Bungeni Dodoma, wakati akijibu swali na Mbunge wa Urambo Mhe.Magreth Sita aliyetaka kujua jinsi Serikali ilivyojipanga kutoa tiba kwa watu wanaong'atwa na mbwa.