Back to top

Watenganisha taka ndani ya dampo Mbeya kuondolewa mara moja.

12 August 2020
Share

Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Musa Sima ameiagiza Halmashauri ya jiji la Mbeya kuwaondoa mara moja watu wanaoingia kwenye dampo la jiji lililopo kata ya Nsalaga, ndani ya bonde la Uyole kwa madai kuwa uwepo wa watu hao ndani ya dampo ni ukiukwaji wa taratibu za uifadhi na utunzaji wa taka kwenye madampo.

Naibu Waziri Sima ametembelea dampo la halmashauri ya jiji la Mbeya na kushuhudia watu wakiwa ndani ya dampo hilo wakiendelea kutenganisha taka ngumu na zile zinazooza haraka hali ambayo hakuridhika nayo na ndipo kuamua kutoa agizo hili.

Mkurugenzi wa NEMC Dk Samwel Gwamaka azitaka halmashauri ya jiji la Mbeya kushirikiana na ofisi yake kutoa elimu kwa wananchi ili wawe wanatenganisha taka hizo punde tu wanapozizalisha.