Back to top

WATOTO 900, WAJAWAZITO 57 WAFARIKI GEITA.

29 April 2023
Share

Zaidi ya watoto 900 na wamama wajawazito 57 mkoani Geita, wamefariki kwa kukoasa huduma za awali za uzazi, wakati wanajifungua katika maeneo yao kwa mwaka jana, hali iliyoilazimu Wizara ya Afya kuja na mpango mpya unaojulikana kwa jina la 'Mmama' utakaowawezesha wajawazito kuhudumiwa na magari maalumu katika maeneo yao ili kuondoa vifo.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa huo,Bw.Martine Shigela, na ksema ukosefu wa huduma umekuwa tishio kwa wakinamama wanaojifungua.

WATOTO 900, WAJAWAZITO 57 WAFARIKI GEITA