
Takriban watu 26 ishirini na sita wamekufamaji na wengine kadhaa hawajulikani walipo, kufuatia ya ajali ya boti iliyotokea eneo la Mokwa, jimbo la Niger, Kaskazini mwa Nigeria.
Msemaji wa Gavana wa Jimbo hilo, Renatus Burashahu, amesema boti hiyo ilikuwa na watu zaidi ya mia moja, wakiwemo wanawake na watoto,ambapo viongozi wa eneo hilo wamesema watu wengine thelathini wameokolewa katika ajali hiyo.
Mwezi Julai mwaka huu, zaidi ya watu mia moja walikufa maji wakati mashua iliyojaa kupita kiasi ilipopinduka katika jimbo la Niger, ikiwa ni moja ya majanga kubwa zaidi katika miaka ya hivi karibuni.