Back to top

Watu 6 wafariki kufuatia ajali iliyohusisha Coaster Segera

05 November 2018
Share

Watu sita wamefariki papo hapo na wengine saba wamejeruhiwa baada ya basi lenye namba za usajili T 124 DHW aina ya Coaster iliyokuwa ikitokea Mkata kuelekea Dar es Salaam kuligonga kwa nyuma lori ambalo lilikuwa limeegeshwa kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo lenye namba za nchi jirani (KDZ 746C) aina ya Fao, katika barabara ya Segera.

Kamishna Msaidizi wa Polisi Wankyo Nyigesa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na amesema Miili ya Marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Bagamoyo ikisubiri uchunguzi.

Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia taarifa zetu.