Back to top

Watu 7 watiwa mbaroni kwa kuhasisha maandamano April 26, Arusha.

24 April 2018
Share

Jeshi la polisi mkoa wa Arusha linawashikilia watu saba akiwemo mwanamke mmoja na watatu kati yao ni wanafunzi wa vyuo vikuu wakidaiwa kuhamasisha maandamano ya tarehe ishirini na sita mwezi huu kwa njia ya mitandao ya kijamii.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Yusufu Ilembo anasema watu hao wamekamatwa  baada ya jeshi hilo kufanya upelelezi wa kiintelijensia na kubaini ushawishi waliyokuwa wanaufanya kupitia mitandao ya kijamii.

Katika kikao na kamanda wa jeshi la polisi baadhi ya waandishi wa habari walitaka kujuwa hatima ya usalama wao endapo kutakuwa na maandano na wao kuamua kufuatilia maandamano hayo.

Katika hatua nyingine kamanda ilembo anasema jeshi la polisi bado linaendelea kumshikilia Askofu mkuu wa kanisa na Internationali Evengelism Church Eliud Isanja anayetuhumiwa kwa kosa la mauaji huku akitoa onyo kwa watu wa jamii ya kifugaji kuto watuma watoto kuchunga mifugo ili kuepuka athari za mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha madhara.