Back to top

Watu 9 wanusurika kifo baada ya ndege kuanguka Mafia, 6 wajeruhiwa.

06 August 2019
Share

Watu 9 wanusurika kifo baada ya ndege ya kampuni ya Tropical iliyokuwa ikiruka kutoka Mafia kuja Uwanja wa Mwalimu Nyerere kuanguka mjini mafia, ambapo watu 6 wamejeruhiwa.

Akizungumza na ITV Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Rufiji Onesmo Lyanga amesema chanzo cha ajali bado hawajakijua hivyo wanaendelea na uchunguzi, huku akisema ndege hiyo ilikuwa inaruka baada ya muda ikashindwa kuruka ndipo ikatokea ajali hiyo.

Amesema kwa sasa majeruhi wa ajali hiyo wamekimbizwa hospitali kupatiwa matibabu baada ya kupata mshutuko kufuatia ajali hiyo lakini jambo la kushukuru hakuna aliyepoteza maisha, lakini ndege hiyo imeteketea na moto.